September 21, 2019


YANGA inafahamu ugumu wa mechi yao ya marudiano dhidi ya Zesco itakayopigwa Jumamosi ijayo hivyo imeanza mikakati mapema na sasa imetuma jeshi la watu sita kwenda kuweka mambo sawa kule Zambia.

Mechi hiyo ya marudiano inatarajiwa kuwa ngumu hasa kwa kuwa mechi ya kwanza walitoka sare ya bao 1-1 na sasa watavaana tena kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia, Jumamosi ijayo.

Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Yanga, Deo Mutta ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa kutambua uzito wa mchezo uliopo mbele yao, Jumanne ya wiki hii jeshi la watu sita lilitangulia Zambia kwa ajili ya kuweka mambo yao sawa bila kutegemea msaada wa Wazambia.

“Tunaimani kubwa ya kwenda kupata ushindi mjini Ndola ndiyo maana maandalizi yetu yameshaanza mapema, wito wetu ni kuhakikisha tunaona vijana wetu wakipambana kwa uhuru katika mchezo huo, maana fitina za mashindano haya tayari tunazifahamu na ndiyo maana tumetanguliza watu mapema.

“Kwa ujumla tunaomba mashabiki zetu watambue kuwa tupo sawa na tumejipanga kwenda kupata ushindi wa hali na mali, hivyo wachezaji wetu wataondoka hapa Septemba 23 (keshokutwa Jumatatu) ili wakazoee hali ya hewa mapema.

“Katika msafara huo wa Jumatatu tunatarajiwa kubeba kila hitaji la msingi likiwemo suala la chakula na maji, tunataka kila kitu kiende sawa,” alisema. Mutta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic