KAMUSOKO AZUA HOFU YANGA
Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuondoka kesho Jumanne kwenda nchini Zambia kupambana na Zesco United katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mashabiki wamepata hofu.
Hofu ya kutofanya vizuri katika mchezo huo imeanza kuwakumba baadhi ya mashabiki wa timu hiyo mara tu baada ya kusikia kuwa mfungaji wa bao la Zesco United katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo uliochezwa Dar es Salaam, Thabani Kamusoko juzi Jumamosi kaifungia tena timu yake hiyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia.
Bao hilo alilifunga dhidi ya Lumwana Radiants na kuiwezesha Zesco United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kutokana na hali hiyo, kipa wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda, ameingiwa na hofu ya timu hiyo kufanya vibaya katika mchezo wake wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii.
Mapunda alisema kuwa uwezo wa juu ambao Kamusoko amekuwa akiuonyesha uwanjani tangu alipotua Zesco lakini pia bao la juzi aliloifungia timu yake hiyo kwa njia ya faulo aliyopiga na kwenda moja kwa moja wavuni, anaona unaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa Yanga kupata ushindi.
“Hofu yangu ipo kwa Kamusoko kwani hivi sasa uwezo wake upo juu na anatishia amani, bao aliloifungia timu yake jana (juzi) ilipokuwa ikicheza dhidi ya Lumwana Radiants lilikuwa bao zuri.
“Alifunga kwa mpira wa faulo ambao ulienda moja kwa moja wavuni, kwa hiyo Yanga wanatakiwa kuwa naye macho sana katika mchezo wa marudiano watakaocheza Jumamosi huko Zambia,” alisema Mapunda.
Jamuna hofu kwasababu Zahera keshafanya hezabu zake na kuhakikisha kuwa timu inakwenda kupinduwa meza
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWatanzania tuwe na akiba ya maneno hii mechi inayokuja siyo rahisi kama mnavyofikiria kwamba Yanga ataingia makundi.....watanzania tunakuwa na matokeo yetu ya "mfukoni na maneno mengi ya kutamba kwamba tunashinda" lakini mwisho wa dakika 90 timu zetu zinatupa matokeo tofauti na mwishowe tunatolewa kwenye mashindano.....halafu tunaanza "nyimbo za visingizio na lundo la vijisababu"....ooh mara "twenzetu ndola tukapindue meza kibabe"....mwisho wa siku mambo yanakuwa tofauti....tunaaminishwa kuwa Yanga atashinda halafu baadaye anatolewa kwa kufungwa.....mimi nashauri tusiongee sana tusubiri mechi ichezwe....ila timu ijiandae kwa ushindani na mapambano ili kuleta matokeo chanya.....tusilishane ujinga na uongo kuwa tunashinda wakati hatujui wapinzani nao wamejipangaje?
ReplyDelete