September 23, 2019


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) amesema kuwa kesho itakuwa na kazi ngumu ya kufanya mbele ya Kenya kwenye mchezo wake wa pili wa michuano ya CECAFA kwa vijana chini ya miaka 20 inayoendelea nchini Uganda.


Ngorongoro Heroes jana ilianza kwa kishindo kwa kuichapa mabao 4-0 timu ya Taifa ya Ethiopia huku Andrew Simchimba akitupia hat-trick yake ya kwanza na Kelvin John naye akifanya yake kwa kufunga bao 1.

“Tumewaona Kenya, ni timu nzuri, uzuri ni kwamba hata wachezaji pia walikuwepo uwanjani na kuona wapinzani wetu wamefanya kitu gani.

 "Utakuwa ni mchezo mzuri na wa ushindani, tunaimani timu yetu itafanya vizuri,” amesema Katwila.

Kwa upande wake beki wa kati wa timu hiyo, Oscar Masai, amesema tayari mwalimu wao amewapa mbinu sahihi za kuikabili Kenya hapo kesho, huku akisisitiza kuwa hali ya wachezaji ni nzuri na wamejipanga kushindana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic