KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na presha kwani
michezo ya Ligi Kuu Bara ipo mingi watafanyia kazi makosa ambayo wameyafanya
mbele ya Ruvu Shooting.
Akizungumza Saleh Jembe,
Zahera amesema kuwa anashangaa mashabiki wanaosema kuhusu kupoteza mchezo wa
kwanza na kusahau kwamba kuna michezo mingi kwenye ligi.
“Ligi haina
mchezo mmoja tukasema imemalizika hapana bado muda wa kufanyia kazi makosa upo
na tutafanya vizuri michezo mingine ambayo imebaki ni suala la kusubiri tu.
“Mpaka sasa
nimeshajua makosa yalipo kwa wachezaji mbali na uchovu ambao ulituponza bado
tuna michezo mingi mkononi hiyo tutafanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu,”
amesema Zahera.
Msimu huu
Zahera amevunja rekodi aliyoweka msimu uliopita kwa kufungwa baada ya mchezo wa
kwanza tofauti na msimu uliopita ambapo alipoteza baada ya kucheza michezo 19
amebakiwa na michezo 37 kufuta makosa yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment