Kiungo wa Simba raia wa Brazil, Gerson Fraga amesema ana imani kubwa na mshambuliaji wa timu hiyo raia mwenzake wa Brazil, Wilker Da Silva kuwa atakapopangwa ataweza kutupia mabao kibao tu katika Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo alisema hayo baada ya kuona uwezo wa mshambuliaji huyo, tangu aliporejea kwenye kikosi hicho. Wilker aliumia nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi hicho cha Simba kwenye mazoezi ya kujiandaa kwa ajili ya msimu huu.
Fraga alisema: “Unajua mimi nina imani kubwa sana na Wilker Da Silva, pamoja na kwamba alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya muda mrefu tangu ayapate wakati tuko kwenye maandalizi, kwa uwezo anaouonyesha mimi naona atafanya makubwa sana msimu huu.
“Zaidi niwaombe tu mashabiki wa Simba wawe na subira na ninawaahidi mambo makubwa kutoka kwa Wilker Da Silva kwa sababu amerejea kikosini akiwa na kasi kubwa ingawa ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu.”
Kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua mshambuliaji huyo, hakuhusika katika mechi yoyote tangu watoke kwenye kambi ya maandalizi ya msimu huu Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment