September 21, 2019


Wakati wakijiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco United ya Zambia, mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amefanikiwa kupunguza kilo nne alizotakiwa kuzipunguza.

Mshambuliaji huyo aliukosa mchezo wa awali wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana tena Septemba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa kwenye Mji wa Ndola nchini huko. Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera alisema amefurahishwa na mshambuliaji wake huyo kufanikiwa kupunguza uzito huo.

“Nataka wachezaji wawe na uzito sahihi ili watimize majukumu yao vyema wakiwa uwanjani, nilianza kwa Molinga (David). “Baada ya hapo nilihamia kwa Balinya ambaye naye uzito uliongezeka kwa haraka mara baada ya ligi ya kwao kumalizika, nimefurahi kumuona akipunguza kilo nne kwa haraka.

“Nilimtaka apunguze kilo haraka, nimpongeze kwenye hilo na tatizo ndiyo sababu ya kwanza kumuweka benchi mchezo wetu na Zesco tuliocheza hapa nyumbani licha ya kuwa na mipango ya kutaka kumtumia kwenye mchezo wa marudiano,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic