KOCHA Mkuu
wa KMC, Jackson Mayanja amesema kuwa kwa sasa ameanza kuwapa mbinu mpya
wachezaji wake ili kupata pointi kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Coastal
Union utakaochezwa Septemba 18.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa wametambua makosa yao kwenye mchezo
uliopita dhidi ya Azam FC ambao walifungwa bao 1-0 wameanza kuyafanyia kazi.
“Kosa letu
kwenye mchezo wa kwanza ilikuwa ni kushindwa kutumia akili kwa wachezaji wangu
na kukosa umakini, tayari tumefanyia kazi makosa na tunaamini tutafanya vizuri.
“Michezo
yetu yote iliyobaki tunahitaji kupata matokeo na hilo linawezekana kutokana na
maandalizi ambayo tunayafanya,” alimema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment