MAMBO yameanza
sasa kwa timu ya Taifa kutafuta tiketi ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la
Dunia ambalo litafanyika mwaka 2022 nchini Quatar kwa sasa ni muda wa kujiandaa
kwa timu ambazo zitapata nafasi ya kushikriki michuano hiyo.
Hii ni
michuano mikubwa namba moja duniani kote na yenye heshima kuliko mingine yoyote
ambayo wacheza mpira huwa wanaifikiria na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA)
huitazama kiupekee katika maandalizi yake na ukamilishaji pia.
Muda huu ni
muda wa kufanya kweli kwa timu yetu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kama
ambavyo imeanza kwenye michuano ya Chan basi ni kuendeleza palepale ambapo
iliishia kutoa burudani kwa mashabiki na Taifa kiujumla.
Wachezaji
wote ambao wameteuliwa kuiunda timu ya Taifa wamepewa kazi ya kuwa mabalozi wa
Taifa kiujumla watambue kwamba wanakwenda kufanya kweli na kuiwakilisha nchi
kimataifa.
Thamani ya
Bendera imejificha kwenye mioyo yao wasisasahau kwamba kuna Watanzania zaidi ya
milioni 20 ambao wanawatazama kwa shauku na kuwaombea dua usiku hata mchana.
Ni leo
Tanzania itakuwa inatupa kete yake ya kwanza kwa kucheza na Timu ya Taifa ya
Burundi hapa sio pa kubeza hata kidogo kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi
maana hawa ndugu zetu na majirani zetu wanatutambua vizuri nasi tunawatambua.
Hii
inatokana na falsafa ya mpira wetu kuwakubli sana makocha na wachezaji kutoka
nchini Burundi jambo ambalo linaleta picha kwamba wao wana kitu kama ambacho
sisi tunacho ni jukumu letu kuonyesha utofauti ili kushinda.
Achana na
suala la Kaimu Kocha kuwa raia wa Burundi hapa leo ni kazi tu kwani tayari
mbinu za Burundi zipo mikononi mwetu basi wachezaji wasipuuzie hata kidogo
mwenyewe amesema kuwa Burundi inabidi wamsamehe yupo kazini kazi iwe kazi
kweli.
Mbinu zote
ambazo wachezaji mnazo zinapaswa leo zitumike kwa ajili ya kuimaliza Burundi
ndani ya uwanja bila kuhofia kwamba mpo ugenini na mwalimu ni raia wa Burundi
matokeo kwanza mengine yatafuata.
Ikukumbukwe
kuwa kwa kuanza kupata matokeo chanya mchezo wa kwanza kutafungua wepesi wa
kazi na njia ya kusonga mbele kwani itakuwa rahisi kupata matokeo chanya nyumbani
wakati wa mechi ya marudio.
Kwa kuwa
tunaanza ugenini hilo halina shida wachezaji kazi yenu iwe moja kupambana
kuzuia lango lisiguswe na mpira hata ule wa kuotea itasaidia kuwa na nguvu kwenye
mchezo wenu wa marudio mtafanya vema na mtapata nafasi ya kusonga mbele.
Picha la
kutisha inabidi lionyeshwe ugenini kwa kucheza kishujaa mwanzo mwisho mpira wa
nidhamu na adabu kwa kuwa mpo ugenini mkitanguliza kiburi mtaumia mapema kabla
mchezo haujaisha.
Makubaliano
yenu wachezaji yawe kwenye kutafuta ushindi na kujituma mwanzo mwisho kwani
Taifa linawategemea katika kuleta furaha siku ya leo kwenye michano mikubwa
ambayo mnashiriki pambaneni bila kuchoka.
Taifa letu
kwenye michezo hatua za kimataifa lipo chini sana hii inatokana na ubovu wa
matokeo kwenye michuano mikubwa sasa kazi inaanza leo mbele ya Burundi
tukipenya tu hapo tayari kuna pointi tutakuwa tumeongeza hapo itakuwa ni furaha
kwa Taifa.
Ikishindikana
kupata ushindi ngoma iwe sare tasa kisha kazi inakuja kumalizwa Taifa kishujaa
kwa sapoti kubwa ya mashabiki mapema tu ushindi upo mikonni mwetu wenyewe
inaitwa tushindwe wenyewe.
Kila la
kheri wachezaji wetu tunaamini kwamba mpo sawa na mnatambua kuwa Taifa
linawategemea tupo bega kwa bega nayi katika mchezo wenu mkubwa na mgumu kwani
kila timu inatafuta matokeo nanyi mnapaswa mfanye kweli.
Hakuna
kulala leo mpaka matokeo yapatikane ndani ya uwanja, chezeni kwa nidhamu
itasaidia kupata ushindi mapema na kutumia uwezo wote ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment