JAMHURI
Kiwelu ‘Julio’ aliyekuwa Kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC amesema kuwa ili
Yanga iwamalize wapinzani wao Zesco mapema inapaswa ibadili mfumo wake wa sasa
wa kuchezesha washambuliaji wengi.
Yanga,
Septemba 14 itakuwa kazini uwanja wa Taifa ikimenyana na Zesco FC uwanja wa
Taifa ikiwa ni mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Julio amesema kuwa Yanga ina kazi kubwa ya kufanya mbele ya Zesco
kutokana na mchezo wao wa kwanza kuwa nyumbani kabla ya kwenda kurudiana na
wapinzani wao ugenini.
“Mtego wa
kwanza ambao upo mikononi mwao ni kwamba wanaanzia nyumbani, wakibugi nyumbani
wataongeza presha kubwa ugenini na kuangukia pua sasa wanachotakiwa kufanya ni
kubadili mfumo ambao wanautumia kwa sasa.
“Ukiwatazama
Yanga wamekuwa na wachezaji wengi wa kigeni ambao wanaunda safu ya ushambuliaji
na wote wamekuwa wakipangwa mbele kufanya ushambuliaji jambo linalowapa ugumu
kupata matokeo, kazi ni ndogo tu Kocha Mkuu apunguze idadi ya washambuliaji
mbele aweke viungo wengi hapo kitaeleweka,” amesema Julio.
HUYU COACH ANA MUONO NA USHAURI WAKE UKIFUATWA TUTAPATA MATOKEO MAZURI
ReplyDeletevizuri kocha, ikiwezekana hata ukhroab awe benchi anarukaruka tu mbele
ReplyDelete