September 12, 2019



KOCHA Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wapo tayari kupambana na Triangel United  kwenye mchezo wa kimataifa kwani wana kazi ngumu ya kufanya kupata matokeo mazuri.

Azam FC, Jumapili itakuwa uwanja wa Chamazi ikimenyana na Triangle United ya Zimbabwe kwenye mchezo wa hatua ya  Kwanza wa Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa anaamini vipaji vya vijana wake wataushangaza ulimwengu kutokana na kile ambacho wamejifunza licha ya ugumu uliopo kwenye michuano ya kimataifa.

"Wachezaji wengi wa Azam FC wamelelewa pale na hii inatupa faraja kwamba ni timu yenye nguvu na ina uwezo wa kupambana bila kukata tamaa, tunatambua haitakuwa kazi rahisi kutokana na wapinzani wetu kujiaandaa.

"Mchezo wetu wa kimataifa ni muhimu kwetu kushinda na tumewapa mbinu kali wachezaji ili kupata matokeo chanya, ni wakati wa mashabiki kuendelea kutupa sapoti kwani kazi ni kubwa na sapoti ni muhimu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic