KOCHA YANGA AWAJIBU TFF KUHUSIANA NA FAINI YA LAKI TANO, ALICHOKIJIBU SASA .......
Baada ya kutozwa faini ya kiasi cha shilingi za kitanzania 500,000, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema yupo tayari kuzilipa.
Jana Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) ilitangaza kumpiga faini hiyo Zahera kutokana na kuvaa mavazi ambayo hayana staha ndani ya uwanja walipocheza mechi ya kwanza ya ligi.
Katika mechi hiyo Zahera alivaa pensi ambayo ndiyo imekuwa sababu ya kupigwa faini na bodi kutokana na kanuni kutoruhusu.
"Mimi nipo tayari kulipa, lakini nashangazwa na kanuni hizi maana ukiangalia nilivaa pensi ndefu ambayo ina heshima.
"Siwezi kukataa sababu wameamua, sasa hivi nitakuwa ninavaa mavazi wanayoyataka maana nina nguo nyingi tu."
Remark
ReplyDeleteMrishindwa kuujaza siku ya wanainchi muujaze siku mtako fungwa kwa aibu kubwa hahaaaa
Sio suala la kuwa na nguo nyingi unatakiwa uwe unavaa vizuri wewe ni kocha wa mabingwa wa kihistoria
ReplyDeleteYeye hupenda kujinata kuwa ana nguo nyingi. Lazima tuseme kweli kuwa Kuboronga Kwa timu katika mechi yake ya kwanza na Ruvu shooting huenda ikawa moja ya sababu Ni yeye pale alipobakia huko Ufaransa bila ya kujali kuwa timu ikijitayarisha na mechi muhimu na kujichelewesha bila ya sababu na kurejea wakati alioutaka yeye mwenyewe na timu kukosea Taalim zake muhimu kwakuwa ndie Kocha mkuu bila ya kiongozi yeyote kushindwa kumkemea kwakuwa anaogopwa na anajuwa kuwa anaogopwa
ReplyDeletebarcelona na chelsea mbona zmefungwa mech ya kwanza tu vp hawakujiandaa? kwan hata mikia ww unafkr itamalza ligi bla kufungwa tena vtoto kagera ndo wanapga mikia nje ndan.shaur zenu yanga ni bigtmu.
ReplyDeleteKufungwa mechi ya kwanza siyo ndo chanzo Cha mtu kukata tamaaa,wanajangwani wenzangu hata 2sikate tamaa hao wengine ni mashabiki maandazi 2
ReplyDelete