Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brigedia Jenerali, Abdallah Mohamed Alphonce, amesema kuwa anaimani na kikosi hicho kuwa kitapindua meza kibabe kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe.
Balozi huyo ndiye aliipokea timu ya Azam FC jana ilipotia timu ofisini hapo kwenda kujitambulisha baada ya kuwasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Septemba 28.
"Nichukue fursa hii kuwakaribisha Zimbabwe na tunaimani kubwa kwamba tutashinda, jinsi ninavyoona mazoezi mnavyofanya naona wachezaji wanafanya mazoezi kwa bidii na wako timamu kwa hiyo tunauhakika kabisa kwamba tutapata ushindi," amesema.
Azam FC ili isonge mbele inahitaji ushindi wa aina yoyote ile kuanzia mabao mawili, baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa 1-0.
Azam FC iliwasili ubalozini jijini Harare, Zimbabwe ikiwa na Meneja wa timu, Luckson Kakolaki, Kocha Msaidizi, Idd Nassor, Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, daktari wa timu, Mwanandi Mwankemwa na Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura, ambaye ni mwakilishi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na mchezaji, Emmanuel Mvuyekure.
0 COMMENTS:
Post a Comment