MAGORI AACHIA NGAZI RASMI SIMBA, CEO MPYA KUTOKA AFRIKA KUSINI ATANGAZWA
Ifisa Mtendaji mpya Simba, Senzo Mazingisa, ametambulishwa leo jijini Dar es Salaam na Crescentius Magori anayemaliza muda wake.
Baada ya utambulisho huo, Magori amesema Mazingisa ataanza kazi rasmi Jumatatu ya wiki ijayo ambapo yeye atakuwa mstaafu.
Magori ameachia rasmi ngazi kufuatia muda wake kumalizika ambapo alipewa nafasi hiyo huku mchakato wa kumtafuta atakayekuwa nafasi hiyo kukamilika.
"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa.
Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu," amesema Magori.








Tanzania ni nchi ya amani duniani.
ReplyDeleteKabla hajaanza kazi atoe tamko la kulaani vurugu zinazofanywa na ndugu zake dhidi ya wageni zinazoendelea huko kwao vinginevyo tutamuweka kwenye kundi moja
ReplyDelete