ZLATAN Ibrahimovic, mshambuliaji wa zamani wa Manchester United amesema kuwa yupo tayari kurejea ndani ya kikosi hicho akimaliza mkataba wake Novemba mwaka huu ndani ya kikosi cha LA Galaxy.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 37 amecheza jumla ya mechi 49 na kupachika mabao 46 akiwa nchini Marekani, kauli hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na United ambapo wametoa sharti jepesi kwake awapigie simu wamalizane.
"Naweza kucheza kwa urahisi sana ndani ya England, kwa hiyo United wakinihitaji nipo tayari kuwatumikia," amesema.
Kabla ya kutumikia Marekani msimu wa mwaka 2016/17 alifunga jumla ya mabao 28 na alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa Ibrahimovic ni mchezaji mzuri kwani licha ya kusumbuliwa na majeraha aliweza kufunga mabao 28.
"Najua anaitambua namba yangu ya simu pia anapajua nyumbani ni wakati wangu kuzungumza naye kama anachosema anamaanisha, ninatambua ni mchezaji mzuri sitashindwana naye," amesema.
United kwa sasa inakwenda kwa mwendo wa kusuasua hasa kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati baada ya kutimka kwa Romelu Lukaku ambaye yupo Inter Milan.
0 COMMENTS:
Post a Comment