ZAHERA AWAJIBU TFF KUHUSIANA NA KANUNI ZA MAVAZI
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa hapa duniani hakuna sheria inayomtaka kocha avae namna gani.
kauli ya Zahera imekuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuja na maboresho ya kanuni ambapo mojawapo ni kuhusiana na suala la uvaaji kwa benchi la ufundi ni lazima uwe smati.
Kanuni hiyo kama ilimlenga Zahera ambaye amekuwa akivaa pensi anapoingia uwanjani timu yake inacheza.
"Duniani kote katika soka hakuna sheria ya mavazi kuwa kocha anatakiwa avaaje, vile mimi navaa nakua relaxed,.
"Kuhusu mavazi Klopp ndiye kocha anayevaa hovyo, ila kama wamebadilisha sheria kwa ajili ya Zahera basi mchezo ujao nitavaa suti."
Hakuna hata mmoja aliekusudia wewe. Ni haki ya TFF kutengeza wanachofikiria kitaleta sura na nidhamu nzuri Kwa timu zetu na hilo halihitajii kupingwa wala hapana aliekusudiwa Ila kuleta sura nzuri ya kupendeza na
ReplyDeletekwengineko huenda ikaigwa na huku imeanzia hapa. Naipongeza TFF Kwa hilo
Nahisi nawe ulikuwepo kwenye utungaji wa sheria hiyo ya mavazi
DeleteUjuha kwani mavazi nini,mwacheni Zahera avae anavyoona inafaa kwake
ReplyDelete