MFAHAMU VIZURI SHIBOUB ALIPOZALIWA MPAKA ANATUA SIMBA - VIDEO
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamedhihirisha hawataki kufanya makosa msimu ujao kwenye ligi hiyo kufuatia kuendelea kujiimarisha walivyoinasa saini ya kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman, aliyekuwa akikipiga Klabu ya Al Hilal ya nchini humo
Shiboub ambaye anajulikana kwa shughuli yake pevu katika idara ya kiungo mkabaji wengi wakimuona kama 'kiungo katili' kutokana na ubora wake katika ukabaji, amekuwa kiungo bora mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan.
Aidha, Shiboub amekuwa akiichezea timu ya Taifa ya Sudan tangu akiwa na umri wa miaka 17, na sasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba.
Shiboub amezaliwa sudan mnamo juni 7, 1994 hadi sasa ana umri wa miaka 25 na nafasi anazocheza ni kiungo na anatumia miguu yote
0 COMMENTS:
Post a Comment