September 1, 2019



BRUNO Tarimo, maarufu kama Vifuaviwili ameibuka mbabe kwa kumyoosha Mserbia, Scheka Gurdijeljac kwenye pambano la ubingwa wa dunia lilofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Serbia.
                                
Ni pambano la 27 kwa Vifuaviwili kucheza na ameshinda jumla ya michezo 26 na kupoteza mchezo mmoja kwa pointi na alitwaa ubingwa wa dunia wa IBF International Super Feather Weights kwa pointi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Vifuaviwili amesema kuwa ni faraja kwake na Taifa kiujumla kufanya vema kutokana na ushindani mkubwa.

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na watanzania pamoja na mashabiki wangu kiujumla nafanya kazi kwa ajili ya Taifa langu, sina cha kusema zaidi ya shukrani.

"Nimeanza safari leo kwa ajili ya kurejea Bongo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho nitawasili majira ya saa 7:00 mchana nikiwa na mkanda wa ubingwa sio kwa ajili yangu bali Taifa," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Asante kwa kuandika habari hii. Wengine hawakuandika kabisa ushindi huu Mkubwa. Watu wameandika tu mapokezi ya bondia aliyeshinda ubingwa wa mabara (Asia Pacific) na kusahau bingwa wa dunia wa IBF wa super feather (Bruno Tarimo)!
    Bruno asikatishwa tamaa na hali hii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic