MILIONI 50 ZAZUA GUMZO YANGA
Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga bado haujawalipa fedha wachezaji wake ambazo ni shilingi milioni 50 za kitanzania.
Yanga waliahidiwa fedha hizo baada ya kuitupa nje Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao 2-1.
Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji hao hawajajua mpaka sasa uongozi umekwama wapi juu ya fedha hizo walizoahidi.
Fedha hizo ziliahidiwa kuwa zitakuwa sehemu ya motisha kwa wachezaji hao ili wazidi kufanya vema katika michuano ya kimataifa.
Hivi sasa Yanga ipo katika maandalizi kuelekea mechi ya hatua ya kwanza dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Inabidi Wapewe Ili Nguvu Ya Kuwatoa Wazambia Iongezeke
ReplyDeleteKwann waahd kama walkua hawana uhakka
ReplyDeleteHii ni sawa na sinema ya kihindi. Mara mchezaji hajalipwa chake huku wachezaji waliahidiwa hajalipwa!! Haya nayo ni kero, viongozi tambueni umuhimu wa wavuja jasho wenu.!!
ReplyDeleteMagazeti yetu haya na jitihada zao kuivuruga Yanga
ReplyDeleteSio kila kitu kisemwe kwa waandishi wa habari
ReplyDeleteMbona kuna taarifa wachezaji walipewa chao wakiwa kule botswana!!��
ReplyDelete