September 1, 2019


Nyota wa mpira wa kikapu, Mtanzania Hashim Thabeet huenda msimu mpya wa Ligi ya Marekani (NBA) akaitumikia moja ya klabu zitakazoshiriki ligi hiyo.

Hashim ambaye amewahi kucheza NBA akiichez Oklahoma City Thunder takwimu zinaonyesha msimu wa 2017/18 aliichezea Yokohama B Corsairs ya nchini Japan.

Sasa, kupitia ukurasa wa Instagram wa timu ya New York Knicks inayoshiriki NBA, ilitupiwa picha ikimuonyesha Hasheem na baadhi ya wadau wa timu hiyo wakiwemo wachezaji na kocha wao wakila chakula cha usiku.

Image result for Hasheem Thabeet New York Knicks
Kwa maana hiyo, huenda Hasheem akadondosha wino wake katika Klabu ya New York au Milwahaukee Bucks kwani mara kadhaa ameonekana akifanya majaribio lakini pia kuonekana katika matukio mbalimbali na wadau hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic