Stars iliyokuwa ugenini ilianza kuruhusu nyavu zake kuguswa mnamo dakika ya 80 kupitia kwa Amiss Cedric baada ya kuwapiga chenga mabeki Stars na kupiga shuti ambalo lilimuacha Juma Kaseja akiwa hana cha kufanya.
Ilichukua dakika tano pekee kwa Simon Msuva kuweza kurejesha bao kupitia mpira wa KAUNTA ATAKI ambayo alimalizia vema langoni mwa Burundi baada ya kipa wao na beki kujichanganya.
Ushindi huo unawapa nafasi ya kufanya vema Stars ambao watakuja kucheza tena na Burundi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Neno suluhu hutumika timu zinapokuwa hazijafungana na ikitokea zimefungana idadi sawa ya magoli kama ilivyokuwa leo basi hiyo huwa ni sare....
ReplyDelete