JESHI la Polisi la Burundi, linamshikilia msimamizi wa masuala ya mechi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Danny Msangi.
Imeelezwa, Msangi na mwandishi mmoja wa habari kutoka Azam TV walishambuliwa na askari hao wakiwemo wanajeshi baada ya kuona wakizuia raia mmoja wa Burundi aliyetaka kupulizia dawa kwenye vyumba vya wachezaji.
"Msangi bado yuko ndani na wameshambuliwa sana kwa ngumi na mateke.
" Walikuwa na Oscar wa EFM, lakini yeye aliachiwa baadaye," kilieleza chanzo.
Stars leo imeibania Burundi kwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza kuwania kucheza Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na bao pekee la Stars lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 85.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba nane uwanja wa Taifa pia kwenye mchezo wa leo Stars hawakuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo muda wa mapumziko.
Dadadeki!!!!!!!!! Hatuhitaji brigade nzima kuwasambaratisha hao wapuuzi,tukituma hata panya road tu wana uwezo wa kwenda kuchafua hali ya hewa,wasituchokoze kabisaaa.Tunawasubiri waje nao wapate kichapo cha "mbwa koko!!"
ReplyDeleteKama kweli hawa wakaulize waganda jinsi tulivyo wapiga vita vya kagera,5 zinasubiri dar mbwa Hawa
ReplyDeleteSoka la Africa Hilo
ReplyDelete