UONGOZI wa
Mtibwa Sugar umesema kuwa kubadilishwa kwa ratiba ya mchezo wao dhidi ya Simba
uliopangwa kuchezwa Septemba 18 na kurudishwa nyuma mpaka Septemba 13 uwanja wa Uhuru haiwazuii wao kuchukua pointi tatu.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hakuna
kitakachowazuia wao kufanya vema kwenye mchezo wao wa pili wa ligi dhidi ya
Simba.
“Timu ikiwa imejiaandaa kutafuta matokeo hakuna kinachoweza
kuzuia kupata ushindi, sasa kwa kuwa ratiba imebadilika kwetu sio tatizo tutawafuata
Simba kwa tahadhari tukizitafuta pointi tatu hata ingekuwa leo hakuna
kinachoshindikana,” amesema Katwila.
Mtibwa
inawasili Dar es Salaam kesho kwa ajili ya kuivaa Simba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Lipuli kwa kufungwa mabao 3-1 na Lipuli FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment