HASSAN Mwakinyo, bondia namba moja kwa Afrika kwenye uzito
wa Super Welterweight kg 69 na namba 19 duniani amesema kuwa hana mashaka na
mabondia kutoka Uingereza wala Marekani ambao wamekubali kupanda ulingoni
kwenye pambano la World Class Fight Tanzania.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika Octoba 26 uwanja wa
Taifa na litarushwa mubashara kwenye baadhi ya vituo vya Televishini vya Bongo
na vile vya nje kutokana na heshima ya Mwakinyo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakinyo amesema kuwa
anatambua kwamba Waingereza na mabondia kutoka Marekani wamepania kupambana
naye jambo linalomfanya ajifue zaidi.
“Wanajua aina ya bondia wanayekwenda kupambana naye ana
uwezo wa aina gani hivyo nao wanajipanga kuonyesha uwezo wao nitawaambua mapema
kabisa kwani nitakuwa nyumbani na mashabiki wangu, hili litakuwa pambano langu
la kwanza nyumbani ni lazima nifanye mambo makubwa.
“Kuhusu kutaja majina yao kwa sasa naliacha suala hilo kwa
mashabiki, kuna majina ya mabondia
kutoka nchi tano ambazo zinahitaji kupambana nami wenyewe watanichagulia
nani nipande naye ulingoni, sapoti muhimu kwa mashabiki,” amesema Mwakinyo.
Watanzania tuko nyuma yako Mwakinyo. Tutakupa sana sapoti siku hiyo. Tunataka knock out iwe katika raundi ya tatu na isizidi hapo.
ReplyDelete