September 2, 2019


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems anampa kiburi cha juu cha kumchapa mpinzani wake George Lwandamina kwenye mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera ataliongoza jeshi la Yanga kupambana na Zesco United ya Zambia kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 14 na kurudiana nchini Zambia.

Zahera ameliambia Spoti Xtra, kuwa; “Mpira wa Congo, Misri na Algeria mpira wao ni mkubwa kuliko Tanzania lakini huko kote Simba walizishinda timu zao.

AS Vita, Al Ahly na JS Saoura walifungwa na Simba kwa nini sisi tusiweze kushinda mbele yao?

“Najua wako juu kimpira lakini hatuwezi kusema kwamba hatuwezi kuwafunga, tutawafunga na kukamilisha kile ambacho tumejiwekea kama malengo yetu.

“Hakuna utofauti baina yetu na hatuwezi kuwaogopa hata kidogo, kitu kikubwa ni kwamba mashabiki waje kutusapoti kwa sababu wao ni muhimu kwetu wakija watatuopa nguvu ya kushinda kwenye mechi yetu hiyo mbele ya Zesco,” alisema Zahera

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic