HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa kikosi chake kimejipanga kupata pointi tatu mbele ya Singida United mchezo utakaochezwa Jumamosi uwanja wa Majaliwa.
Namungo yenye maskani yake Lindi kete yake ya kwanza ilishinda mbele ya Ndanda FC kwa mabao 2-1 itamenyana na Singida United ambayo ilipoteza mbele ya Mwadui FC.
"Wachezaji wana morali kubwa na nina imani tutafanya vema kwani tulianza vizuri ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment