AZAM FC kwa
sasa ipo nchini Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa
kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Triangel United na Serikali ya
Tanzania kupitia ubalozi wake nchini humo umeipa sapoti.
Kaimu Balozi
wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brigedia Jenerali, Abdallah Mohamed Alphonce
ambaye aliipokea timu ya Azam almesema kuwa ana imani na kikosi hicho kinaweza
kupindua meza kibabe.
“Nitumie
fursa hii kuwakaribisha Zimbabwe na nina amini kwamba kwa namna nilivyoona
maadalizi ya kikosi kuna uhakika mkubwa wa kupata matokeo kwenye mchezo wa
marudio,” amesema.
Ofisa Habari
wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa maandalizi ya mwisho yapo
vizuri na wana imani ya kupata matokeo chanya.
Ili Azam FC
isonge mbele kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 28 uwanja wa
Barbourfields ni lazima ishinde mabao zaidi ya mawili baada ya kufungwa bao 1-0
mchezo wa kwanza Bongo.
0 COMMENTS:
Post a Comment