September 20, 2019




Hauwezi kuamini kuwa wachezaji nyota wa Rwanda, Patrick Sibomana na Meddy Kagere wamekutana wakiwa katika jezi za klabu zao.

Wawili hao, Sibomana akiwa amevaa jezi ya Yanga pamoja na Deus Kaseke huku Kagere akiwa amerupia rangi ya nyekundu na nyeusi yaani Simba wamekutana katika kusherehesha droo mpya ya wadhamini wao SportPesa.

Kazi hiyo ya kuitangaza droo mpya ambayo itatoa zawadi ya gari mwishoni lakini kutakuwa na zawadi za simu ambazo zitamwagwa kila Jumatano kwa ambao wanabeti.

Kila Jumatano sasa kampuni ya mambo ya kubeti ya SportPesa, itakuwa ikifanya droo na waliobeti kujishindia simu.

Mshambuliaji nyota wa Simba, Meddy Kagere naye alipata nafasi ya kuingia ndani na kujaribu utamu wa zawadi kubwa ya mwisho wa drop hiyo ambayo ni gari la kisasa.



kama hiyo haitoshi, droo kubwa itafuatia na mshindi ataibuka na mchuma mpya ambao wachezaji wa Yanga, Patrick Sibomana na Dues Kaseke nao walijitokeza na kuushuhudia.

Mkurugenzi wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema wanaendelea kuwajali wapenda mpira na wateja wao na wameshirikiana na kampuni ya Tigo kufanya mambo yawe moto zaidi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic