SELEMAN
Matola, Kaimu Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa amesema kuwa wanaingia uwanjani
leo kuwavaa wapinzani wao Burundi kwa tahadhari kubwa lengo likiwa ni kufanya
kweli.
Stars leo
itamenyana na Burundi mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la dunia 2022
nchini Quatar utakaopigwa uwanja wa Prince Louis Rwagasore kabla ya kurejeana
nao Septemba nane uwanja wa Taifa.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa
wanatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila wana imani ya kufanya vema.
“Mchezo wetu
ugenini hautakuwa mwepesi hilo tunalitambua na tumelifanyia kazi kwa ukaribu,
wachezaji wote wanajua kwamba jukumu lao ni kutafuta matokeo kwani tunahitaji
kumaliza kazi huku kabla ya kurejea nyumbani.
“Kila kitu kipo sawa na morali ni kubwa na malengo yetu makubwa ni kuona tunafanya kweli kwa kupata matokeo chanya, mashabiki watupe sapoti,” amesema.
TFF buana mnaleta raha! Hivi wenzangu macho yenu yanaona kama yangu? Nawaona kocha mkuu, msaidizi na meneja wakiwa katika vazi style ya Zahera vile! Kifungu na kanuni zilizotumika kumwadhibu Zahera juu ya dhana ya mavazi yasiyo ya heshima ni kwa vilabu pekee au mpaka national team? Shame upon us
ReplyDelete