MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa wachezaji wanatambua kazi kubwa ambayo wametumwa na Taifa kwa ajili ya kupeperusha bendera mbele ya Burundi.
Stars leo inaanza safari ya kwenda nchini Burundi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Quatar.
Samatta amesema:'Stars ni timu ya watanzania wote na kila mmoja anatambua kwamba wachezaji tumepewa jukumu la kufanya kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Taifa tupo tayari kwa ajili ya kupambana na kupata matokeo chanya licha ya kuwa tutakuwa ugenini," amesema.
Mchezo wa wa kwanza utachezwa kesho Septemba nne nchini Burundi na ule wa marudio utachezwa Septemba nane uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment