September 7, 2019


UONGOZI wa Yanga umemtaka beki wa kati, Andrew Vicent ‘Dante’ kuripoti kambini kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Zesco ya Zambia.

Beki huyo inaelezwa amegomea kujiunga na timu hiyo kutokana na kudai fedha zake za usajili wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara ambazo ni shilingi milioni 45.

Timu hiyo juzi Jumatano ilisafiri kwenda mkoani Mwanza kwa ajili ya kambi ya pamoja huku ikiwa mkoani humo ikitarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuvaana na Zesco, Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, ameliambia Championi Ijumaa kuwa juzi katika kikao cha Kamati ya Utendaji, suala la Dante lilijadiliwa na kufikia muafaka alipwe fedha zake haraka mara zitakapopatikana.

Mwakalebela alisema kuwa kabla ya kulipwa fedha hizo, Dante anatakiwa aripoti kambini kuanza mazoezi ya pamoja ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Zesco.

Aliongeza kuwa, Dante siyo mchezaji pekee anayeidai Yanga, wachezaji wengi wanadai wakiwemo wengine ambao wamehama, lakini amewahakikishia watalipwa.

6 COMMENTS:

  1. Tunasikia kuwa Yanga Kwa sasa inaoga mabilioni ya shilingi ikiwa Ni kweli kwanini inashindwa kuwalipa haki zao na huku wakikiri kuwa wachezaji wengi hawajalipwa. Mlipe kibaruwa wachezaji haki yake kabla ya kukauka jasho lake

    ReplyDelete
  2. walijitamba sasa wamepata utawala mpya kumbe wapi hata kujali maslai ya wazawa wameshindwa

    ReplyDelete
  3. duuh umuhimu wke hawauni kwa xx lakn wakumbeke jinsi alivyoipgania team 2018/2019 bongo bahati mbaya

    ReplyDelete
    Replies
    1. tutaacha wengi pia wazuri.tutabaki na wachache pia waby.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic