October 23, 2019


Ukiweka kando Bongo Fleva, Muziki wa Hip Hop Bongo kwa zaidi ya miaka 20 umeweza kusimama bila kupotea.

Wapo wasanii mmoja mmoja wanaoendelea kuutetea muziki huu ambao unagusa hisia na kueleza uhalisia huo uliopo mitaani kwetu tunapoishi kila siku.

Katika makala haya, nimekuandalia orodha ya wasanii 10 ambao wanaonekana kukishika kiwanda cha muziki wa Hip Hop Bongo.

FID Q

Anajulikana pia kama Fareed Kubanda. Ni kati ya marapa wanaoinyanyua na kuishikilia gemu ya Muziki wa Hip Hop Bongo.

Anatikisa kwa sasa na albamu yake ya Kitaa Olojia ambayo aliifanyia uzinduzi miezi miwili iliyopita.

P THE MC

P the MC anaingia katika listi hii akiwa anafanya kazi zake nyingi akiigusa jamii moja kwa moja kama vile Ngoma ya I Miss You, Baba Msaliti, Askari Msela na nyingine kibao.

Kwa sasa rapa huyu anabamba na Ngoma ya Binti aliyomshirikisha, Suraiya inayoelezea maisha halisi ya mabinti wanaotokea kwenye mazingira magumu Bongo.

NIKKI MBISHI

Wengi wamezoea kumuita Baba Malcom kutoka kikosi cha Tamaduni Music kinachobeba wasanii wengine wa Hip Hop.

Nikki ni aina ya marapa Bongo wanaosimamia wanachokiamua na kwa sasa yupo mbioni kuja na kichupa cha ngoma yake ya Welcome 2 Gamboshi (W2G).

ONE THE INCREDIBLE

Unaweza pia kumuita Moko Miujiza akimaanisha namba ndogo inayoongoza namba nyingine zote.

Amekuwa akifanya uhalisia wa maisha ya mtaani kwenye muziki wake na pia kwenye filamu ambazo anazicheza.

MEX CORTEZ

Ni raia wa Tanzania mwenye asili ya Sri-Lanka huko barani Asia.

Amedumu kwa muda wa miaka mitatu mpaka sasa ambapo anasumbua na Ngoma ya Kokoriko akiwa na Fresh pamoja na One the Incredible.

BLUE

Huwezi kumuacha njiani mkongwe huyu kwenye gemu la Hip Hop Bongo.

Mr.Blue alianza kuimba kisha akahamia kwenye muziki wa Hip Hop kwa kuandika mistari ya kugusa hisia za watu wengi.

Kwa sasa anasumbua na Ngoma ya Hatutaki Kesi huku akiwa amemshirikisha Rich Mavoko.

SONGA

Moja kati ya jambo pekee alilonalo ni uwezo wake wa kuchana kwenye mashindano ‘rap battle’ ambayo amekuwa akishindanishwa na wasanii wengine wanaofanya Hip Hop Bongo ambapo amekuwa akiwashangaza wengi sana kwa jinsi anavyokuwa na floo tofauti kila inapofika zamu yake.

Kwa sasa mkali huyu anatamba na Ngoma ya Pombe Siyo Chai.

MWANA FA

Ni miongoni mwa marapa waliousogeza Muziki wa Hip Hop Bongo hadi kufika hapa ulipo.

Mwana FA au Binamu kama ambavyo wadada wengi wamezoea kumuita, kwa sasa anasumbua na ngoma ya We Endelea Tu.

MSAMIATI

Ni zao kutoka kijiwe cha MJ Records kinachoakisi maana halisi ya Muziki wa Hip Hop Bongo.

Anasumbua na ngoma yake ya Macho Kodo aliyomshirikisha Ben Pol.

YOUNG LUNYA

Ni kati ya marapa bora kabisa wachanga kuwahi kutokea Bongo ambaye alikuwa mmoja wa wanaounda Kundi la OMG chini ya Quick Rocka lakini kwa sasa anafanya kazi kama Solo Artist akiwa na kazi mpya inayotambulika kama Moto.

4 COMMENTS:

  1. Mkuu kafanye zaidi utafiti hiyo list yako itakua poa zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli asee hzi tafiti hazipo ktk uhalisia inaonesha kakurupuka t

      Delete
  2. umekurupuka jomba kuna marapa wakali wapo kwenye game tangu miaka ya tisini joh makin jcb chindo man profesa jay kina jay mo uwaoni

    ReplyDelete
  3. Kwangu kuna rapper mwingine kutoka OMG anafahamika kama CONBOI huyu jamaa ni shida aisee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic