IKIWA leo Simba na Azam
FC zinashuka Uwanja wa Taifa jijini Dar kumtafuta mbabe atakayebeba pointi tatu
muhimu kwenye mchezo wa ligi, rekodi zinaibeba Simba.
Mpaka sasa Azam FC
ambayo imepanda daraja msimu wa mwaka 2008, imekutana na Simba mara 22 kwenye
michezo ya ligi kuu na katika michezo hiyo Simba imeshinda mara nyingi zaidi
kuliko Azam FC.
Katika michezo hiyo,
Simba imeshinda jumla ya mechi 9 huku Azam FC ikishinda mechi 6 na zimetoshana
nguvu michezo 7.
Katika mechi zote hizo hakuna mchezaji aliyefanikiwa kufunga
hat trick kwenye mchezo mmoja.
Jumla ya mabao 45
yamepatikana katika mechi hizo 22 ambapo Simba imefunga jumla ya mabao 26 na
Azam FC ikifunga mabao 19.
Msimu wa kwanza
walipokutana mwaka 2008, Azam FC iliitungua Simba mabao 2-0. Wafungaji ni Jamal
Mnyate dakika ya 42 na Shekhan Rashid dakika ya 90.
Matokeo yao ya jumla
yalikuwa namna hii:-2008-09 Azam 2-0 Simba, Simba 3-0 Azam FC. 2009-10, Simba
1-0 Azam FC, Azam FC 0-2 Simba. 2010-11 Azam 1-2 Simba, Simba 0-2 Azam. 2011-12,
Simba 0-0, Azam 0-2 Simba. 2012-13, Simba 3-1 Azam FC, Azam 2-2 Simba.
2013-14, Simba 1-2 Azam
FC, Azam 2-1 Simba.
2014-15, Azam 1-1 Simba, Simba 2-1 Azam FC. 2015-16, Simba
2-2 Azam FC, Simba 0-0 Azam FC. 2016-17, Azam 0-1 Simba, Simba 0-1 Azam FC
2017-18, Simba 0-1 Azam
FC, Simba 0-0. 2018-19 Simba 3-1 Azam, Simba 0-0 Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment