October 31, 2019


IKIWA ni saachache baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutangaza kuwa Meneja wake, Babu Tale ameshafanya mawasiliano na Menejimenti ya msanii mwenzake, Alikiba kuhusu ushiriki wake wa kwenye tamasha la Wasafi Festival litakalofanyika Novemba 9, jijini Dar es Salaam, Alikiba naye amemjibu Diamond tena kwa ghadhabu.

Kiba kupitia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Diamond kwa kuandika, “Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME)

Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz,“.

Hii ni mara ya pili kwa Alikiba kukataa kutumbuiza kwenye tamasha hilo la Wasafi Festival, alifanya hivyo pia mwaka jana ambapo alisema yupo tayari kutoa udhamini kupitia kinywaji chake cha Mo faya badala ya kufanya shoo.

6 COMMENTS:

  1. Huyu jamaa mkimya sana halafu hana mambo ya kiishowshow na kiajabuajabu,ye anaangaliaga mambo yake hata hashobokeagi kuponda watu,ukiona hivyo ujue Kuna jambo kubwa kavumilia naona akiwashe tu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni matako tu uyo hana lolote tatzo lake ana umimi sana

      Delete
  2. Kwa hiyo mwizi anapewa kazi ya kutafuta alichokiiba? Duuuh

    ReplyDelete
  3. Haya majibu ya kiba yanaonyesha bado hajakua. Anautoto mwingi kichwani.

    ReplyDelete
  4. Kiba anajitambua pia ni mtu ambae ashobokei vp well done brother

    ReplyDelete
  5. hahaha kama amedinda ameze wembe,,,,mamaqeee hajitambui,.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic