ZAHERA ALIPUA TENA BOMU LINGINE YANGA, AZUNGUMZIA HATMA YA MKATABA WAKE
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hawezi kuwasikiliza mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC bali anawasiliana na uongozi ambao ulimpa mkataba.
Hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kutoa malalamiko yao wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayosema yamekithiri kwenye kikosi ikiwemo kushindwa kupanga vizuri kikosi cha kwanza pamoja na mbinu.
“Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwahiyo siku viongozi wakinitaka kiwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini”, amesema Zahera.
“Nina uzoefu mkubwa ila hapa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yoyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids FC na lingine ni kwamba wakati tunasajili wachezaji, hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika ila tulisajili kwa ajili ya ligi”, ameongeza.
Aidha, Zahera amesema kuwa mashabiki hawapaswi kumlaumu yeye kwa matokeo ya Klabu Bingwa kwani kikosi chake kiliandaliwa kwa ajili ya ligi kuu, ambako hawapo katika nafasi mbaya mpaka sasa, wakiwa wamecheza mechi chache.
Yanga inatarajia kusafiri hadi nchini Misri kuvaana na Pyramids katika mchezo wa marudio utakaopigwa wikiendi hii, ikiwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-1.
Nahic Zahera hajui kupangilia sentensi ndio maana anashindwa kujitetea. Zahera aliamini tunaenda kutolewa na Township Rollers ndio maana aliwatupia uongozi lawama ya kambi ya Moshi na Arusha. Zahera nina wasiwasi na ufanisi wake ndio maana akifungwa anawatupia lawama viongozi wa timu, TFF na sehemu zingine husika. Zahera si fundi wa mpira ila ni fundi wa hamasa. Kongo imefanya vibaya kwenye mashindano....alafu ananiambia yeye ni fundi. Zahera anataka kuniambia kama timu ikichukua ubingwa atawaondoa wachezaji wote ili asajili upya wachezaji wa mashindano ya Afrika. Zahera hakosi sababu ndio maana aligoma mkataba wa Buildcom kwa kuogopa kushindwa kuwasiliana yaani lugha kama anavyotumia lugha ya kiswahili kutulaghai mashabiki, wanachama na viongozi wa Yanga. Juma Balinya ni mchezaji bora kabisa pale Uganda hata Kocha wa Pyramids alimtaja kama ndio hatari.....Farouk Shikalo ndio golie bora kwenye ligi ya Kenya na mshiriki wa Kimataifa.....Lamine Moro ni beki bora kutoka ligi ya Zambia, Patrick Sibomana na Winga matata kutoka timu ya Taifa ya Rwanda na timu ya Mukura Victory, Kelvini Yondani ni Beki bora wa Tanzania, Juma Abdul ni Fullback bora wa miaka miwili iliyopita na bado ana kiwango bora. Ally Mtoni Sonso ni fullback bora kutoka lipuli iliyocheza fainali ya kombe la Azam, Pappy Tshishimbi ni mido bora kutoka Mbambane Swallows (Iswatini), Balama Mapinduzi aka Kipenseli ni mido bora kijana kwenye kiwango cha sasa, Maybin Kalengo ni Striker bora kutoka Zesco United, Makame na Faisal ni mido bora kutoka Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Herroes)....wewe ni nani unaesema kuwa hakuna mchezaji anayeweza kucheza Pyramids au kimataifa????
ReplyDeleteHivi visingizio havina mashiko. Hawa wote niliowatafa ni very experienced football players in Tanzania and everybody know that. Kocha muongo sana. Atoe sababu zingine.
Vyura umaneni
ReplyDeleteKweli vyura viumane sasa.nouma na busy!!!!
Delete