October 27, 2019


ACHANA na matokeo, lakini Azam FC wameweka rekodi na heshima ya aina yake kwa kuchezesha wachezaji saba kwenye mechi dhidi ya Simba ambao wamewatengeneza wenyewe pale Chamazi.

Wachezaji hao saba wamekulia kwenye kituo cha kukuza vipaji cha timu hiyo yenye uwanja wake wa kisasa wa Azam Complex.

Simba asilimia kubwa ya wachezaji wao wamenunua kwa gharama kubwa kutoka ndani na nje ya nchi.

Walioanza kwenye kikosi cha kwanza ni kiungo Mudathir Yahya, winga Joseph Mahundi ambao wote walionyesha kiwango. Lakini mastaa wengine watano walikuwa benchi wamekulia Azam na wameiva kwa kucheza mechi zozote kubwa.

Hao ni kipa Benedict Haule, mabeki Abdul Omary, Oscar Masai, kiungo Masoud Abdallah na mshambuliaji Shaban Chilunda.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Azam imepewa zawadi ya mamilioni ya shilingi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kama kuwapongeza kwa program zao makini za kukuza vijana.

5 COMMENTS:

  1. Acha unafiki kwenye mechi ya azam na Simba, Azam alichezesha wachezaji wengi wa kigeni kuliko wazawa.

    ReplyDelete
  2. Muandishi kanjanja,endelea kupiga promo ila mnyama ndio anaendelea kutetea ubingwa wake.

    ReplyDelete
  3. https://1.bp.blogspot.com/-jQpgzlHH_d4/XbBQauGSAUI/AAAAAAAAWSc/epO_YAZzKVESu_6KKiUY0cRWTqOrgmstACLcBGAsYHQ/s1600/mauajii.PNG

    ReplyDelete
  4. Achaga uongo brother,kumbuka azam imechezesha,bruce kangwa,wadada,yakubu,chirwa,daniel amo,donald ngoma na wengine kibao wageni tafuta kikosi utakiona achaga uongo brother.

    ReplyDelete
  5. Sasa hiyo rekodi gani? Mbona mnapenda sana kulazimisha stori za rekodi? Ovyoooo...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic