October 19, 2019


LICHA ya Diego Costa nyota wa Atletico Madrid kupachika bao la kuongoza dakika ya 36 kwa mkwaju wa penalti halikufua dafu kwao kusepa na pointi tatu mbele ya Valencia.

Mchezo huo uliopigwa leo ambao ni wa La Liga umeshuhudiwa ukimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku yote yakiwa ni ya mipira iliyokufa.

Daniel Parejo alipiga bonge moja ya faulo akiwa nje ya 18 uliozama mazima ndani ya lango dakika ya 82 na kuweka mzani sawa.

Lee Kang nyota wa Valencia dakika ya 90+1 alionyeshwa kadi ya njano kabla ya VAR kutengua na kuonyesha kuwa alipaswa kuonyeshwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa na mwamuzi wa mchezo.

Matokeo hayo yanaifanya Atletico Madrid kuwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 huku Valencia ikiwa nafasi ya sita na pointi 13 zote zimecheza mechi 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic