October 20, 2019


Yamemkuta! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwimbaji wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha kuingia kwenye utata baada ya kuonekana klabu akicheza muziki na warembo.

Mbasha yamemkuta kwa sababu chama cha muziki wa Injili cha Tanzania Music Foundation (TAMUFO) kimeapa kumchukulia hatua kali endapo itabainika kweli yeye ndiye yupo kwenye video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha akiwa klabu akichezewa muziki kihasara na warembo.

Akizungumza na Shusha Pumzi, katibu mkuu wa chama hicho, Stella Joel alisema taarifa hizo wamezipata na mastaa wengi wa Injili wamechukizwa na kitendo hicho hivyo wao kama viongozi wapo kwenye uchunguzi wa tukio hilo na ikibainika kwamba ni kweli, Mbasha atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Shusha Pumzi ilimtafuta Mbasha ili kujua ukweli wa video hiyo akiwa klabu na alipoulizwa alijibu kwamba siyo kweli na ile video iliyosambaa mitandaoni ni ya kutengenezwa tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic