October 16, 2019



AZAM FC imedhamiria kulipa kisasi mbele ya Simba kwa kuanza kuonyesha makeke kwenye mechi za kirafiki kabla ya kuvaana na Simba, Octoba 23 uwanja wa Uhuru kwa kuipoteza safu ya ushambuliaji ya Simba kwa kucheka na nyavu mara nyingi zaidi.

Simba na Azam zinajiandaa na mchezo wa ligi wameanza kucheza michezo ya kirafiki kujiweka sawa baada ya ligi kusimama.

 Simba imecheza michezo miwili na Azam FC pia imecheza michezo miwili na zote hazijapoteza mchezo hata mmoja huku safu ya Azam FC ikionekana ina makali zaidi ya ile ya Simba ndani ya dakika 180.

Mchezo wa kwanza kwa Simba ilikuwa dhidi ya Bandari ya Kenya uwanja wa Taifa na ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na kiungo Ibrahim Ajibu huku Azam FC wao wakipachika mabao 5-0 mbele ya Green Warriors na mabao yalifungwa na Kassim Khamis alitupia mabao mawili, Donald Ngoma, Richard Djod na Seleman Ndikumana wakitupia bao mojamoja.

Mchezo wa pili Simba ilicheza na Mashujaa ya Kigoma na ilipata ushindi wa bao 1-0 lilipachikwa na kiungo, Sharaf Shiboub huku Azam FC ikishinda mabao 2-0 mbele ya African Lyon uwanja wa Uhuru wafungaji wakiwa ni Idd Kipagwile na Joseph Mahundi.

Ndani ya dakika 180 ambazo timu zote mbili zimecheza, Simba imefunga mabao mawili yaliyofungwa na viungo huku safu ya ushambuliaji ya Simba ikiwa haijaambulia bao hata moja na Azam FC ikifunga jumla ya mabao saba na washambuliaji wamefunga mabao matatu pekee.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wake wanadharau mechi za kirafiki jambo linalowafanya washindwe kupata matokeo makubwa ambayo wanayahitaji.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa bado anaendelea kukijenga kikosi chake kwa sasa ili kiwe bora zaidi.

2 COMMENTS:

  1. Statistically your very poor kwa vile ulitakiwa uangalie wachezaji wa ngapi wako national team

    ReplyDelete
  2. Simba imechezesha wachezaji 6 ws kikosi cha pili , ambacho na ambacho Azam akiwa kamuli anafungwa za kutosha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic