BALINYA ATAJWA KINYANG'ANYIRO MCHEZAJI BORA UGANDA
Imeripotiwa kuwa straika wa kimataifa wa Yanga, Juma Balinya, ametajwa kuwania nafasi ya Mchezaji Bora wa mwaka nchini Uganda na chama cha soka nchini humo (FUFA).
Nyota huyo aliyesajiliwa Yanga msimu huu akitokea timu ya Polisi ya nchini humo, ni miongoni mwa wachezaji vipenzi kwa mashabiki wa Yanga licha ya kwamba hadi sasa hajaonyesha cheche zake za kupachika mabao.
Taarifa imeeleza kuwa Balinya ameingia katika nafasi tano za juu sambamba na nyota wengine akiwemo Allan Okello, Denis Onyango, Timothy Awany na Patrick Kaddu.
Aidha Balinya kupitia ukurasa wake wa Instagram, amewaomba mashabiki wake kumpigia kura ili aweze kushinda kinyang’anyiro hicho.
“Nichukue nafasi hii kuwaomba mashabiki kunipigia kura ili niweze kushinda kwenye nafasi hii muhimu kwangu,” alisisitiza Balinya.
Balinya aliisaidia Yanga kuvuka hatua ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufunga bao muhimu katika mchezo wa ugenini dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana iliyomalizika kwa ushindi wa bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment