BEKI SIMBA AANGUKA MAZOEZINI, APATWA NA KIZUNGUZUNGU, ASHINDWA KUONA
Katika hali isiyo ya kawaida juzi beki wa Simba Tairone Santos alianguka mazoezini ghafla kutokana na kupatwa na kizunguzungu.
Beki huyo alianguka wakati Simba wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kuanguka kwake kulilipa wakati mgumu jopo la madaktari wa timu hiyo kutokana na kushindwa kuelewana lugha ya kuzungumza.
Kudondoka kwa Tairone kulimfanya alalae chini na kushindwa kuona, hali ambayo ilikuwa si ya kawaida.
Jopo hilo la madaktari likiongozwa na Yassin Gembe lilianza kumpatia huduma Tairone na mpaka kiungo Gerson Fraga alipoitwa eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia kuwaelewesha mawasiliano waweze kujua tatizo lililomkumba.
Baada ya kutokea tukio hilo, Tairone aliondolewa uwanjani akiwa bado hajaanza kuona huku ratiba zingine za mazoezi zikiendelea.
Daktari Gembe alisema: "kilichotokea kwa Tairone si jambo la kushtua, ni hali ya kawaida kwa mchezaji, hii ilisababishwa na jua kuwa kali kitu ambacho kilisababisha apatwe na kuzunguzungu kisha kushindwa kuona.








Misumali ya Mlipili hiyo!
ReplyDelete