PASCAL Wawa, beki kisiki wa Simba ambaye mwili aliwahi kucheza Azam FC amesema kuwa mechi tatu za kirafiki walizocheza ambazo ni sawa na dakika 270 zinawapa nguvu ya kupambana na Azam FC kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Oktoba 23 uwanja wa Uhuru.
Simba ilianza kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Bandari uwanja wa Uhuru ikashinda kwa bao 1-0 kisha ikakwe pipa kuwafuata Mashujaa ikashinda bao 1-0 kabla ya kulazimisha sare mbele ya Aigle Noir ya Bandari.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa namna kikosi kilivyocheza michezo ya kirafiki kumeongeza morali ya wachezaji kupambana pamoja na kuzoea mfumo mpya.
“Hatuna kingine ambacho tunakifikiria kwa sasa, kikosi kimecheza michezo mingi ya kirafiki jambo ambalo limetufanya tuwe na muunganiko mzuri, ni wakati wetu kuonyesha kile tulichojifunza kwa vitendo katika michezo yetu yote ikiwa ni pamoja na huu dhidi ya Azam FC,” amesema.
Seleman Khamis, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wana imani ya kupata matokeo chanya mbele ya Simba kutokana na maandalizi waliyopata.
“Tumecheza michezo mingi ya kirafiki ambayo imetufanya tuwe imara kwa sasa, muunganiko wetu umekuwa imara, tupo vizuri na tutapambana kupata matokeo chanya kikubwa sapoti ya mashabiki,” amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment