BAADA ya kukusanya pointi 12 ndani ya dakika 360 hesabu zinazompasua kichwa kwa sasa, Patrick Aussems raia wa Ubelgij ndani ya Simba ni dakika 270 za mwezi mpya Octoba.
Simba itaanza kuzisaka pointi tatu Octoba 23 uwanja wa Uhuru dhidi ya Azam FC kisha itasafiri mpaka Singida na itacheza Octoba 27 Uwanja wa Namfua, Singida dhidi ya Singida United na mchezo wa tatu mwezi huu itakuwa Octoba 30 Uwanja wa Kambarage jambo linalompasua kichwa Aussems kutokana na ushindani uliopo ndani ya Ligi.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hesabu kubwa za Simba ni kuendeleza furaha kwa mashabiki kwa kupata matokeo chanya kwenye michezo yao yote.
"Tunatambua ushindani ni mkubwa nasi tunajipanga kufanya vizuri, benchi la ufundi kiujumla lina kazi ya kufanya kuona namna gani timu itapata matokeo," amesema.
Aussems amesema kuwa kikubwa anachohitaji ni ushindi kwenye michezo yake yote ya ligi msimu huu licha ya ushindani kuwa mkubwa jambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment