October 4, 2019


Meneja Masoko wa Kampuni ya Star Media (T) Limited, David Malisa ameweka bayana kuwa kwenye Chaneli zao za  michezo zilizopo kwenye king’amuzi  cha  StarTimes, zimeanza  kuonyesha michuano mikubwa barani Ulaya ya kufuzu Euro 2020 na Europa League.

Mbali na hayo Malisa amesema kwamba kupitia michuano hiyo mtumiaji yeyote wa king’amuzi hicho ataweza kushuhudia mechi kadha wa kadha za timu kubwa za England kama vile Manchester United inayochezewa na Marcus Rashford na Arsenal ya straika Pierre Emerick Aubameyang.


Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes, David Malisa (kushoto) akimkabidhi jezi Shaffih Dauda.

Kupitia michuano hiyo pia Malisa amesema kuwa wamelazimika kuingia kwenye ushirikiano na Mtangaza nguli wa michezo nchini Shaffih Dauda, ambaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha anawachambulia baadhi ya michezo wateja wa StarTimes kutokana na uelewa wake katika mambo hayo ya soka.

“Tunafahamu kuwa sehemu kubwa ya Watanzania ni wapenda soka, hivyo kuanzia siku ya Alhamisi (jana), tungependa walipie vifurushi vyao kwani wataanza rasmi kushuhudia mechi kadhaa za Europa League ambapo Shaffih Dauda atakuwa na jukumu la kuchambua na kuwahabarisha baadhi ya mambo yahusuyo soka kupitia mitandao yake ya kijamii lakini hata kupitia StarTimes,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic