October 21, 2019


Kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa hakuna kitu kitachomzuia beki kitasa na nahodha wa kikosi hicho Aggrey Morirs kucheza kwenye mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Simba.

Morris alikuwa nje kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti, baada ya kuumia kwenye majukumu ya timu ya taifa, ambapo alianza mazoezi mepesi zaidi ya wiki moja iliyopita na juzi alikuwa sehemu ya kikosi cha Azam kilichoichapa Transit Camp mabao 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Cheche alisema; “Hakuna kikwazo cha yeye kushindwa kucheza kwa hivi sasa, hivyo niwaambie mashabiki wa Azam kuwa, Aggrey ameshapona na atacheza kwenye mchezo wetu na Simba.”

Azam wapo katika maandalizi makali kuelekea katika mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Simba, utakaopigwa Oktoba 23 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

1 COMMENTS:

  1. Kumzuia dhidi ya simba kwani yeye ni nani?hata akiwepo ataongeza nini?ilivyochapwa na mnyama mpaka wakamfukuza kocha alifanya nini na alikuwepo uwanjan,acheni kutengeneza influence isiyo na tija,the time will tell acha tusubiri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic