October 19, 2019


Katika kuhakikisha wanafanikiwa kuibuka na ushindi hapa nyumbani dhidi ya Pyramids ya nchini Misri, uongozi wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa, umeandaa kikosi kazi kwa ajili ya mchezo huo.

Kwanza kabisa kikosi kazi hicho kinafanya majukumu ya kuwachunguza wapinzani wao ili kujua ni jinsi gani wanaweza kuwakabili.

Yanga inatarajia kushuka dimbani Oktoba 27 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuvaana na Pyramids katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya Mtoano katika Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo tayari kikosi kazi hicho kimeshatua jijini Mwanza kwa ajili ya kambi hiyo ili kuzoea mazingira ya huko.

Yanga imefika hatua hiyo ya kucheza mechi mbili za mtoano baada ya kuondolewa katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-2.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema wamekuwa wakiwafuatilia wapinzani wao kwa ukaribu zaidi kwa kuunda jopo maalumu la kikosi kazi kuhakikisha wanawashinda wapinzani wao kwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani.

“Tunahitaji kufanya vyema katika mchezo wetu dhidi ya Pyramids kwa kuutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani, tumeandaa jopo maalumu la watu kwa ajili ya kuwachunguza wapinzani wetu, tunahitaji kufanya vyema.

“Tunahitaji kujua eneo gani wapo dhaifu na eneo gani wapo vizuri ili tuweze kufanyia kazi, lengo ni kuhakikisha tunakiimarisha kikosi chetu,” alisema Mwakalebela.

Zahera arejea Yanga na mbinu mpya Naye, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana Alhamisi alitarajiwa kutua nchini kuendelea na majukumu yake ya kukinoa kikosi cha timu hiyo akitokea kwenye majukumu yake ya kuinoa timu ya taifa ya DR Congo.

Imeelezwa kuwa amerejea na mbinu mpya atakazozitumia ili kuhakikisha Yanga inapata ushindi CCM Kirumba.

Taarifa za ndani kutoka kwenye uongozi wa Yanga zinaeleza kuwa Zahera amekuja na mbinu tofauti kwa kuwa katika michezo iliyopita hawakuwa na matokeo mazuri lakini mchezo huo dhidi ya Waarabu ni muhimu kwao kumaliza kila kitu katika ardhi ya nyumbani.

Alipotafutwa Kocha Msaidizi wa Yanga, Mzambia, Noel Mwandila ili kujua mikakati yao, alisema: “Kuna mbinu mpya, tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mchezo wetu huo wa kimataifa.

“Kuna mambo mengi ambayo tuliyabaini tulipocheza dhidi ya Zesco tayari tumeshayafanyia kazi, pia tutakuja na mfumo mwingine katika mechi hiyo ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic