October 18, 2019


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi juu ya dhamana  ambayo walifutiwa waliokuwa viongozi wa Klabu ya Simba kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwa amemaliza kuandaa uamuzi wa shauri hilo. 

Shauri hilo linasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo awali alipanga kutoa uamuzi lakini kumbe muda alipanga ulikuwa mfupi kuweza pitia uamuzi huo.

Hakimu huyo alitakiwa kutoa maamuzi kwa mara nyingine kuhusiana na kuwafutia mashitaka ya utakatishaji fedha washitakiwa wawili Evans Aveva na Godfrey Nyange ambayo yaliwapa nafasi ya kupata dhamana. 

Hata hivyo maamuzi hayo ya awali ya Hakimu Simba yalipigwa na serikali ambapo walikata rufaa Mahakama Kuu kuomba maamuzi ambayo yalitolewa yote yaweze kutenguliwa huku upande serikali ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa serikali, Wonkyo Saimon. 

Simba ameahairisha kesi hiyo hadi Oktoba 25, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya kesi hiyo. 

Ikumbukwe wiki iliyopita mahakama ilitoa uamuzi na kuwafutia mashitaka mawili ya utakatishaji fedha waliokuwa viongozi wa Simba lakini baada serikali ilikata rufaa juu ya maamuzi hayo.

Ikumbukwe Aveva na Kaburu washitakiwa kwa makosa tisa, mawili yakiwa ni ya utakatishaji fedha pamoja na mengine ya kughushi ambapo aliunganishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic