October 12, 2019


Inaelezwa kuwa aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa klabu ya Simba, Crescentius Magori anaweza akatangazwa kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi (TPLB).

Magori ameanza kutajwa kuchukua nafasi hiyo kwa bosi wa sasa ambaye ni Boniface Wambura ambaye inaelezwa atapangiwa majukumu mengine ya kazi.

Magori alipewa nafasi ya Uofisa ndani ya Simba kwa muda wa miezi sita ambao hivi sasa tayari umeshamalizika na sasa anatajwa kuchukua nafasi ya Wambura pale Bodi ya Ligi.

Bado Simba na Bodi ya Ligi hawajaweka wazi ju ya uwepo wa tetesi hizi lakini Saleh Jembe Blog itazidi kufuatilia mpaka mwisho wake kuujua ukweli.


4 COMMENTS:

  1. Nendeni tu mkainyooshe yanga maana ndio mnachokijua na si kupeleka mbele soka letu...

    ReplyDelete
  2. Yanga wanajinyoosha wenyewe kwa mipango mibovu. Timu mbovu, uongozi legelege na visingizio kibao.Wananikumbusha Simba Simba ya 2015.Ni kosa la wengine wote lakini sio lao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nyie mnamipango gani ambayo ni endelevu,lipeni kwanza hela ya usajili kwa baadhi ya wachezaji wenu,mkiambiwa wachezaji wanaidai club mnakasirika na kutishia kuwashtaki watu,kudaiwa inadaiwa nchi ijekuwa club,acheni mikwara ya abunuwasi nyie

      Delete
  3. Wachezaji wamewapeleka mpaka TFF na FIFA kwa madeni.Umesikia hao wachezaji wanadai?Kama anavyofanya Dante,Pato nä Mwinyi?
    Kitu cha radio chini ya mwanachama wenu Maulid Kitenge wanajaribu kuzua ili kutuliza mambo.Mnashika mashati kila siku.Hali itakuwa mbaya zaidi mtakapochapwa na waarabu.Ruvu keshawatungua .Polisi nä Coastal mmebebwa lakini mtakiona cha moto mtapokutana na timu nzuri zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic