October 12, 2019



FRED Minziro, ‘Baba Isaya’ aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Singida United amesema kuwa alishasoma alama za nyakati ndani ya Singida United zilizompa taa nyekundu jambo ambalo halijamshangaza kuskia ametangazwa kocha mpya.

Miziro aliinusuru Singida United kushuka daraja msimu uliopita wa mwaka 2018/19 ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia pointi 46 ilishinda michezo 11 na kutoa sare 13 na kupoteza jumla ya michezo 14.

Minziro amesema kuwa kupigwa kwake chini kisha Ramadhan Nsanzurwimo kurithi mikoba yake halijamshtua.

“Unajua wengi hawaelewi namna mambo yanavyokwenda kwenye soka letu la Bongo, ila hilo halinipi presha kwani wao wanaendelea na mambo yao nami ninaendelea na mambo yangu.

“Kwa mwenendo ambao nilikuwa naenda nao nilitambua kitakachotokea na kuna baadhi ya mechi niliziacha kama ile ya Namungo sikuwepo kabisa, yote kheri maisha lazima yaendelee,” amesema Minziro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic