October 4, 2019


Baada ya Yanga kulazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania jana, Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa watulivu kipindi hiki.

Yanga ilikuwa na kibarua hicho jana cha mchezo wa ligi ukiwa na wa pili baada ya mechi ya kwanza kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Nugaz alisema kuwa bado ni mapema mno kuanza kutupia lawama benchi la ufundi kwasababu timu imecheza mechi mbili pekee.

"Nawaomba wanayanga wote wawe na subira kwani timu ndiyo kwanza imeshacheza mechi mbili pekee.

"Ligi nayo ndiyo kwanza haijapamba moto, ni vema tukawapa wachezaji na benchi la ufundi muda ili waweze kufanya kazi yao," alisema Nugaz.

Matokeo ya jana yameifanya Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria kunako Ligi Kuu Bara kufikisha kuwa na alama moja na ikiwa mkiani mwa msimamo.

4 COMMENTS:

  1. Nyie viongozi ndio mnasababisha wanachama wakarike,mnasema tutashinda 3/0. Sasa imekuaje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakuna ukakasi wowote kwa kiongozi kusema tutashinda 3 bila.
      ishu wachezaji wana utimamu kiasi gani, Kocja Zahera kuna vitu anakosa katika fslsafa yake kimpira ambayo inachangia matokeo kuwa mabovu.

      atumie muda mwingi kufikir namna ya kuifanya yanga kuwa na taswira mpya.
      ndicho alichoanza nacho patrick aussens. alipoamua kuijenga timu,hakudeal na mashabiki, wala wapambaji, hakudeal na viongoz wala wapnzaj, alideal na wachezaji, na alipoona kuwa kicha masud anamchezea akili ali muondosha, sasa zahera anacheza na akili ya mashabiki na viongozi, anacheza na media, anasahau kaz yake ni kufundisha mpira wa kisasa.

      yanga ninyi ndio mnampa.sba ubingwa kirahisi na si vingine, kama mwanzo wa ligi mech 2 mnapata point moja,mwenzenu mechi 4 anapoint 12 na goñi zaid ya 10!
      mnataka kubisha ukwel kuwa simba ndio klabu bora kwa sasa hapa tz?

      Delete
  2. huyo Nugaz mwambie ana mimba nini kwahiyo mechi ya township walicheza wale sio yanga na zesco nae kwann aseme mechi mbili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic