MORGAN Schneiderlin kiungo wa zamani wa Manchester United amejutia uamuzi wake wa kusepa mapema ndani ya kikosi hicho.
Schneiderlin alisepa kwenye kikosi cha United mwaka 2017 na kujiunga na Everton baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Hata hivyo kiungo huyo amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Everton na kuona kuwa hakustahili kusepa mapema ndani ya United.
"Nadhani kwa sasa sina la kufanya zaidi ya kupambana kurejea kwenye ubora wangu na kupata namba zaidi huku niliko.
"Naona kuwa nilishuka mapema kwenye boti kabla haijafika jambo ambalo limekuwa likiniumiza kwa sasa, nadhani nilipaswa kusubiri na kupambana kupata namba ndani ya United nawaangalia wachezaji wengi namna walivyo kwa sasa na mafanikio yao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment